Aslay aonyesha namna ambavo anajiamini kwenye muziki wake, anataka kuachia wimbo

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: aslay-aonyesha-namna-ambavo-anajiamini-kwenye-muziki-wake-anataka-kuachia-wimbo-863-rickmedia

Aslay hataki kujua kuhusu wasanii wakubwa (Diamond Na Alikiba) kuachia nyimbo zao kwamba ni tishio kwa wasanii wengine, awauliza mashabiki zake kama wako tayari kuupojkea wimbo wake mpya kwani anatamani kuachia wimbo mpya ijumaa hii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram (Insta Story) Aslay ameandika "Najisikia kama nitoe ngoma hii iIjumaa, Mnaonaje?"

Sio wasanii wote wanaojiamini kutoa nyimbo wakati Alikiba na Diamond wakiwa kwenye promotion ya nyimbo zao lakini Aslay imani yake ni kubwa sana kwa mashabiki zake na ndio maana anajisikia kuachia ngoma ijumaa.

Ukipewa nafasi ya kumshauri utamruhusu atoe wimbo Ijumaa hii au asubiri kidogo wakubwa wamalizane na watu wao?