Loading...

Davido ampeleka Mama Mtoto Wake wa kwanza Mahakamani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 weeks ago
rickmedia: davido-ampeleka-mama-mtoto-wake-kwanza-mahakamani-132-rickmedia

 Staa wa muziki kutoka Nchini Nigeria #Davido amemfungulia Mashtaka mahakamani Mzazi mwenzie Sophia Momodu, mama wa mtoto wake wa kwanza, Imade.

Katika ombi la msingi lililowasilishwa na mawakili wake, Dk Olaniyi Arije, Okey Barrah na wengine, katika Mahakama Kuu ya Jimbo la Lagos, tarehe 17 Aprili 2024, Davido aliiomba mahakama hiyo amri ya kutoa ulinzi wa pamoja wa Mtoto wao Imade Adeleke.

Staa huyo anaiomba mahakama itoe amri kutolewa vikwazo vya kumona Mtoto wake bila kizuizi chochote.

Davido anasema kutokana na upendo kwa mwanae aliamua kumpa nyumba Momodu yenye thamani ya N200m (Tsh.Milioni 350) huko huko Oniru, Kisiwa cha Victoria, Lagos lakini ilikataliwa.

Mbali na hivyo Staa huyo anasema aliamua kumnunulia Mtoto wake Gari aina ya Range Rover SportUtility kwa ajili ya matumizi yake na Mama (Mlalamikiwa).