Kanye West Amebadilisha Jina Lake Tena na Sasa ni YE YE

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 days ago
rickmedia: kanye-west-amebadilisha-jina-lake-tena-sasa-108-rickmedia

Rapa #KanyeWest (YE) Amebadilisha jina lake tena baada ya miaka minne tangu abadilishe jina lake kutoka #Kanyewest mpaka #YE Kisheria.

Kwa mara nyingine rapa na mjasiriamali wa mitindo amelibadilisha tena jina lake na kuwa Ye Ye, kulingana na nyaraka mpya za biashara zilizopatikana huko California.

Kulingana na Page Six, afisa wake mkuu wa fedha , #HussainLalani, aliwasilisha nyaraka zinazoonyesha mabadiliko hayo.

Jina jipya, “Ye Ye,” sasa linaorodheshwa katika kampuni yake kadhaa ikiwemo Yeezy Apparel, Yeezy Record Label LLC, na Getting Out Our Dreams Inc.

West hapo awali alitumia jina “Ye West” katika usajili wa awali.