Rapa Ofset apigwa risasi akiwa nje ya Cassino huko Florida Marekani

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 hour ago
rickmedia: rapa-ofset-apigwa-risasi-akiwa-nje-cassino-huko-florida-marekani-861-rickmedia

Rapper Offset amelazwa hospitali baada ya kupigwa risasi nje ya casino moja nchini Florida, Marekani, huku polisi wakiwakamata watu wawili kuhusiana na tukio hilo.

Kwa mujibu wa taarifa, msanii huyo ambaye jina lake halisi ni Kiari Kendrell Cephus alipigwa risasi Jumatatu katika eneo la maegesho ya magari (valet) nje ya hoteli na casino ya Seminole Hard Rock.

Msemaji wake alithibitisha kuwa kwa sasa yuko hospitali akipatiwa matibabu na hali yake ni nzuri, huku akifuatiliwa kwa karibu na madaktari.

Maelezo kuhusu chanzo cha tukio hilo hayajatolewa mara moja. Hata hivyo, idara ya polisi ya Seminole ilisema watu wawili wamekamatwa na uchunguzi unaendelea.

Polisi waliongeza kuwa eneo hilo liko salama na hakuna tishio kwa umma, huku shughuli zikiendelea kama kawaida.

Tukio hilo limekumbusha kifo cha aliyekuwa rapper mwenzake kwenye kundi la Migos, Takeoff, aliyefariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kupigwa risasi nje ya ukumbi wa bowling mjini Houston.