Rayvanny atembelea nyumbani alikozaliwa msanii wake 'Kus Love'

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: rayvanny-atembelea-nyumbani-alikozaliwa-msanii-wake-kus-love-366-rickmedia

Wasanii wengi mara nyingi huwa wanatoke maisha ya chini kabisa na baadaye wao ndio huwa wanakuja kubadilisha hali ya kiuchumi nyumbani na kufanya ndugu zao waneemeke na vipaji vyao, sasa historia inajirudia kwa msanii mpya wa Rayvanny pale Next Level Music 'Kuss Love' (Nyumbani kwao pia hali ya maisha ni ya kawaida sana)

Kwenye kipande cha video alicho-share Rayvanny kwenye ukurasa wake wa Instagram kinawaonyesha wakiwa na msanii wake mahali ambapo msanii wake amekulia na ni nyumbani kwao, Kuss ameweka wazi kuwa hali ya maisha kwao ni duni na kwasasa yeye ni yatima (Wazazi Wote wamefariki).

Hii sio hadithi mpya kwa jamii ya kitanzania lakini haimaanishi ni jambo la kulichukulia kawaida na ndio maana Rayvanny ameamua kumshika mkono kijana huyu ili aweze kutimiza ndoto zake za kubadilisha maisha ya nyumbani kwao.

Kuss Love tayari ameachia Extended Play (EP) aliyoipa jina la 'Gold' yenye jumla ya nyimbo sita huku akiwa amemshirikisha boss wake 'Rayvanny' kwenye nyimbo mbili tu.

hii ni project ya kwanza kwa msanii kuiachia tangu atangazwe rasmi kama msanii wa Next Level Music, yeye anakuwa msanii wa pili kuwahi kupita kwenye mikono ya Rayvanny baada ya Mac Voice kupita kwenye lebo ya Next Level Music.