Kupitia ukurasa rasmi wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amesema kuwa tayari ametoa maelekezo rasmi ya kisheria kufuatia picha na video zinazosambaa zikimwonyesha mtu anayejulikana kama "AnkoT" akiwa na mwonekano wa kike.
Waziri Dkt. Gwajima amebainisha kuwa mhusika huyo amepuuza elimu aliyopewa awali na BASATA kuhusu maadili ya kazi za sanaa, hivyo hatua zinazochukuliwa sasa zinalenga kuhakikisha "ajali ya kisheria" inaandaliwa kwa umakini ili wahusika wasiponyoke Mahakamani.
Dkt. Gwajima amewataka wananchi kushirikiana na Serikali kwa kukusanya ushahidi wa picha na video za watu wanaomomonyoa maadili mtandaoni ili kusaidia upelelezi unaoendelea.
Amesisitiza kuwa, licha ya kero inayosababishwa na vitendo hivyo, mamlaka zinahitaji kufuata miongozo ya kitaalamu na kisheria badala ya mihemko, ili kuhakikisha wale wote wanaokaidi maoni ya jamii na utamaduni wa taifa wanatiatia hatiani kwa mujibu wa sheria zilizopo.