Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imemhukumu kunyongwa hadi kufa Bw. Godlisten Anandum Lema (42) mkulima, Mkazi wa Kata ya Usariver Wilaya ya Arumeru baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mke wake Bi. Esther Rumishael Massawe.
Akisoma hukumu hiyo Machi 16, 2026 kesi namba 15185 ya mwaka 2025 Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Frank Mahimbali alisema Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pasipo shaka yoyote na kumtia hatiani mtuhumiwa huyo.
Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 08, 2024 muda wa saa 12:00 asubuhi huko katika maeneo ya Lakitatu, Kijiji cha Mlimasioni, kata ya Usariver wilayani humo kabla ya kufikishwa Mahakamani na kupatikana na hatia.