Loading...

Raia Sita wa Morocco wahukumiwa kifo nchini Somalia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 month ago
rickmedia: raia-sita-morocco-wahukumiwa-kifo-nchini-somalia-147-rickmedia

Mahakama ya Kijeshi Kaskazini mwa Somalia imewahukumu adhabu ya kifo raia 6 wa Morocco kwa kile kilichoelezwa wana uhusiano na Kundi la Kigaidi, pamoja na hivyo wahusika wana nafasi ya kukata rufaa, ikitokea wakashindwa adhabu itatekelezwa kwa kupigwa risasi hadi kifo.

Majina ya wahusika ni Mohamed Hassan, Ahmed Najwi, Khalid Latha, Mohamed Binu Mohamed Ahmed, Ridwan Abdulkadir Osmany na Ahmed Hussein Ibrahim.

Wakati huohuo, Mahakama imewahukumu raia wa Ethiopia na Somalia, vifungo vya Miaka 10 gerezani kila mmoja kutokana na kuhusika katika kesi hiyo. Mwendesha Mashtaka wa Mahakama amewaambia Waandishi wa Habari kwamba raia wa Morocco walikamatwa Puntland kufuatia uchunguzi uliofanyika kwa Mwezi mmoja.