Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa zinazoweza kusababisha mafuriko kwa muda wa siku tatu kuanzia Jumatano hadi Ijumaa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Aprili 7, 2026, mvua hizo zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Lindi na Mtwara, pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
TMA imeeleza kuwa uwezekano wa mvua hizo na athari zake uko katika kiwango cha kati, lakini imeonya zinaweza kusababisha mafuriko na kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi.
Wananchi wametakiwa kuchukua tahadhari muhimu ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.