Waajiri wapigwa marufuku kukata kodi ya pango kwa watumishi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: waajiri-wapigwa-marufuku-kukata-kodi-pango-kwa-watumishi-957-rickmedia

Wabunge leo Juni 9, 2025 wamepitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa mwaka 2025, wakati wa kikao cha 42 cha mkutano wa 19 wa Bunge la Bajeti jijini Dodoma.

Muswada huo umefanyiwa marekebisho mbalimbali ikiwemo vifungu vya 12 na 13 vilipendekezwa kurekebishwa kwa lengo la kuondoa wajibu wa mwajiri kukata kodi ya nyumba pamoja na faini ya kuchelewesha kodi, kutoka kwenye mshahara wa mfanyakazi ambaye ni mpangaji wa nyumba za shirika hilo.

Kwa mujibu wa utaratibu unaopendekezwa waajiriwa watalipa kodi ya pango kama ambavyo wapangaji binafsi wanalipa. Lengo la marekebisho haya ni kuongeza uwajibikaji wa moja kwa moja kwa mpangaji katika kulipa kodi ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi za nyumba za shirika hilo.