Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la kimataifa la wahamiaji la Umoja huo IOM vifo vya takriban watu 1,000 vimeripotiwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, na kuufanya kuwa mwaka ulioshuhudia vifo vingi zaidi tangu mwaka 2014.
Shirika hilo limeyataja matukio mbali mbali ya kuzama kwa meli ikiwemo tukio la Jumapili lilosababisha kutoweka kwa wahamiaji 80 baada ya boti walimokuwa, kuzama wakitokea Libya. Tangu tarehe 28 March watu wasiopunguwa 180 walifariki au hawajulikani waliko kufuatia matukio matano tofauti ya meli kuzama.