Aliyeteuliwa na Trump kuwa kama Waziri wa Ulinzi Peter Hegseth anakabiliwa na tuhuma za unyanyasaji wa kingono baada ya Mwanamke mmoja wa California kudai kuwa aliwahi kuwa nae kwenye chumba cha hoteli ambapo alichukua simu yake kwanguvu na kumyanyasa kingono
Ripoti ya polisi iliyotolewa hivi karibuni ya Mwaka 2017 inafichua maelezo mapya kutokana na tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya mteule wa waziri wa ulinzi wa Trump.
Kwa mujibu wa maelezo ya wakili wake amedai kuwa Hegseth hakushtakiwa kwani aliingia kwenye makubaliano ya suluhu na mshtaki wake ambayo yalijumuisha malipo ya fedha na kusisitiza kwamba mkutano huo ulikuwa wa makubaliano, wakili huyo alisema alikuwa na hofu kwamba mwanamke huyo alikuwa tayari kutoa madai dhidi yake
Msemaji wa timu ya mpito ya Trump Karoline Leavitt pia alidai kwamba polisi waligundua madai hayo kuwa ya uongo na kumwita Hegseth "Mkongwe wa Vita anayeheshimika sana ambaye ataitumikia nchi kwa heshima atakapothibitishwa kama Katibu ajaye. wa Ulinzi, kama yeye kwa heshima aliitumikia nchi yetu kwenye uwanja wa vita kwa sare."alisema Leavitt.
Mbali na hivyo Rais mteule Donald Trump amemteua aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Florida Pam Bondi kama mteule wake mpya wa kugombea Idara ya Sheria.
Awali Trump alimteua Matt Gaetz, ambaye alijiondoa Novemba 21 alhamisi ambae anakabiliwa na uchunguzi baada ya kamati ya maadili ya Bunge kutoa ripoti kuwa Gaetz alijihusisha kingono na ulawiti kwa binti mwenye umri wa miaka 17 na matumizi haramu ya dawa za kulevya, alikubali zawadi zisizofaa, alitoa upendeleo maalum kwa mawasiliano ya kibinafsi na kujaribu kuzuia juhudi za serikali kumchunguza.