The Guardian Yasitisha Kupandisha Maudhui Kwenye Mtandao Wa X

-rickmedia: Lanka Ting

Lanka Ting

2 months ago
rickmedia: the-guardian-yasitisha-kupandisha-maudhui-kwenye-mtandao-426-rickmedia

Shirika la Habari la #TheGuardian limetangaza kwamba halitachapisha tena maudhui kwenye mtandao wa kijamii wa #ElonMusk, X, kutoka kwenye akaunti zake rasmi.

Katika tangazo kwa wasomaji wake Jumatano, Novemba 13, shirika la habari hilo lilisema kuwa manufaa ya kuwa kwenye mtandao huo, ambao awali uliitwa #Twitter, sasa yamezidiwa na athari hasi, ikitaja maudhui yenye kutia hofu yanayopatikana humo.

"Tulipenda kuwafahamisha wasomaji kwamba hatutachapisha tena kwenye akaunti zozote rasmi za uhariri za The Guardian kwenye tovuti ya kijamii ya X," limesema shirika hilo.The Guardian ina zaidi ya akaunti 80 kwenye X zikiwa na takriban wafuasi milioni 27.

Shirika hilo lilisema maudhui kwenye mtandao huo yanajumuisha nadharia za njama za mrengo mkali wa kulia na ubaguzi wa rangi. Aidha, liliweka wazi kuwa namna tovuti hiyo inavyoshughulikia uchaguzi wa rais wa Marekani imethibitisha uamuzi wake.

Makundi yanayopinga hotuba za chuki na Umoja wa Ulaya yamekosoa Musk, mtu tajiri zaidi duniani, kuhusu viwango vya maudhui kwenye mtandao huo tangu alipojinunulia kwa dola bilioni 44 mwaka 2022.