Mchezo wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya #Simba ikiwa nyumbani dhidi ya #CSSfaxien ya Tunisia umemalizika kwa wenyeji kushinda magoli 2-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Simba ambayo ilipata Goli lake kupitia kwa Kibu Denis aliyesawazisha baada ya Haj Hassen kutangulia kufunga kisha kuongeza la pili kwa mfungaji yuleyule dakika za nyongeza, imefikisha Pointi 6 katika michezo mitatu ya Hatua ya Makundi.
Simba inatarajiwa kuwa ugenini kurudiana na CS Sfaxien mnamo Januari 5, 2025.