Mwanamke aliyedai ni mama mzazi wa msanii Bahati akataa majibu ya DNA Test

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

10 hours ago
rickmedia: mwanamke-aliyedai-mama-mzazi-msanii-bahati-akataa-majibu-dna-test-828-rickmedia

Mwanamke anayedai kuwa mama mzazi wa mwanamuziki wa Kenya, Bahati amekataa matokeo ya kipimo cha DNA yaliyotolewa jana ambayo yalionyesha kuwa hakuna uhusiano wa kibaolojia kati yake na msanii huyo.

Katika video aliyoipost msanii bahati kwenye mtandao wake wa Instagram inamuonyesha mwanamke akilia kwa uchungu huku akisisitiza kuwa Bahati ni mtoto wake wa kumzaa licha ya ripoti ya kitabibu kuonyesha vinginevyo.

Kwenye video hiyo pia, Bahati anaonekana pamoja na daktari wakijaribu kumtuliza mwanamke huyo huku wakimbembeleza baada ya kushtushwa na majibu ya maabara.

Kwenye video nyingine mwanamke huyo ameendelea kusisitiza kuwa anamfahamu Bahati kama mtoto wake na kudai kuwa matokeo hayo hayawezi kubadilisha kile anachokiamini na anajua kuna kitu kinaendelea ila msisitizo ni ule ule kuwa yeye ndiye mama mzazi.

Ukipita kwenye maoni katika video hizo alizopost Bahati watu wengi wanaona kama ni maigizo tu (Kutafuta Kiki) na baadhi \ya watu wanasema "kweli mama huyu hana Bahati" na baadhi wanasema Bahati angemuasili tu mama huyu.

Maoni yako ni yapi kwenye hili??