Mtoto apoteza jicho moja baada ya kubusiwa kwenye jicho na mtu mwenye virusi

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: mtoto-apoteza-jicho-moja-baada-kubusiwa-kwenye-jicho-mtu-mwenye-virusi-596-rickmedia

Nafikiri umewahi kusikia wataalamu wa afya mbalimbali wakisisitiza kuwa si salama kumbusu busu mtoto kwani ni rahisi kumuambukiza magonjwa mbalimbali, sasa huenda kisa hiki kikakufungua zaidi na kukemea zaidi tabia hiyo kama na wewe ni mmoja kati ya wengi wenye tabia hiyo.

Mwaka 2025, mtoto wa miaka 2 Uingereza aliyeitwa Juwan alipoteza uwezo wa kuona, jicho lake kushoto baada ya kuambukizwa na virusi vya herpes simplex aina 1 (HSV‑1). Maambukizi haya yalitokea baada ya kupigwa busu na mtu aliye na dalili za virusi hivyo vilivyosambazwa kwenye jicho lake.

Mwanzo madaktari walidhani ni maambukizi ya kawaida ya jicho, lakini hali yake ilizidi kuwa mbaya. Baada ya uchunguzi zaidi, daktari aligundua kuwa alikuwa na herpes simplex keratitis, ugonjwa hatari unaosababisha vidonda kwenye kornea na kupoteza kuona.

Kwa bahati mbaya, licha ya matibabu na upasuaji, jicho lake limeharibika na uwezo wa kuona umepotea. Familia yake imetoa ujumbe wa tahadhari kwa wazazi kuepuka kumbusu au kuwasiliana kwa karibu na mtu aliye na dalili za maambukizi, kwani virusi vya HSV‑1 vinaweza kuwa hatari sana kwa watoto wadogo.