Diamond Platnumz na wenzake wampa Baba Levo Madawati 857

-rickmedia: Rick

Rick

1 hour ago
rickmedia: diamond-platnumz-wenzake-wampa-baba-levo-madawati-857-47-rickmedia

Kampeni ya Mbunge wa Kigoma Mjini Baba Levo kuhakikisha jimbo lake linamaliza tatizo la madawati mashuleni imeanza kuonesha matokeo chanya hii ni mara baada ya kutazanga kupokea zaidi ya madawati 800 kutoka kwa wasanii na wafanyabiashara.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Baba Levo ameandika kuwa "MPAKA SASA NIMEPOKEA MADAWATI 857 KUTOKA KWA WASANII NA WAFANYA BIASHARA 🙏🙏🙏. LENGO NI KUFIKISHA MADAWATI 2500 KWA AWAMU YA KWANZA ..!!

MAHITAJI YA KIGOMA MJINI NI MADAWATI 8,000"

Baba Levo anazidi kuweka alama jimboni kwake akiwa kati ya Wabunge wenye kuvutia wapiga kura wake kutokana na juhudi zake za kuleta mabadiliko ndani ya Jimbo lake la Kigoma Mjini. Ukiachilia mbali swala la madawati, Baba Levo ameshaanza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha rami.