Mkurugenzi wa uendesha vipindi EFM na TVE 'Ssebo' afariki Dunia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

11 hours ago
rickmedia: mkurugenzi-uendesha-vipindi-efm-tve-ssebo-afariki-dunia-578-rickmedia

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uendeshaji na Biashara wa EFM na TVE, Denis Busulwa, maarufu (Ssebo), amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumatano, Machi 11, 2026 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi wa EFM na TVE, Francis Majizo, kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, akieleza kuwa taratibu za awali za msiba zinaendelea na taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

"Bwana ametoa, Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe,".