Mchezaji Avunja Uchumba siku 3 baada ya kumvalisha Pete mpenzi wake

-rickmedia: Rick

Rick

3 days ago
rickmedia: mchezaji-avunja-uchumba-siku-baada-kumvalisha-pete-mpenzi-wake-380-rickmedia

Ulimwengu wa soka na mashabiki wa mahusiano nchini Costa Rica na Guatemala wameachwa na mshangao baada ya nyota wa soka, Derrikson Quiros, kutangaza kuvunjika kwa uchumba wake siku tatu tu baada ya tukio la kihistoria la kuomba kuvalisha pete ya uchumba Uwanjani.



Quiros, ambaye anakipiga katika klabu ya Xelaju nchini Guatemala, aligonga vichwa vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuandaa tukio la kimahaba mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi ya Kitaifa (Clausura).

Hata hivyo, "hadithi hiyo ya ngano" imeingia doa mapema mno. Zikiwa zimepita saa 72 pekee tangu pete hiyo ivaliwe, Quiros ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza mwisho wa mahusiano yao, jambo lililozua maswali mengi miongoni mwa wafuasi wake.

Licha ya kuandika Ujumbe huo Quiros hajaweka wazi sababu za kubadili maamuzi yake.