Zimebaki siku chache tu kabla ya msimu kumalizika, lakini safari ya mshambuliaji raia wa Ghana, Jonathan Sowah, ndani ya klabu ya Simba imefika tamati mapema zaidi.
Taarifa za ndani zinaeleza kuwa mkataba wa Sowah na Simba umevunjika baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano ya kuachana. Sowah, ambaye hakuonekana uwanjani kwenye mechi za ligi tangu Desemba 7, 2025, anasemekana kuchoshwa na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kumbukumbu ya Sowah: Alijiunga na Simba msimu huu akitokea Singida Black Stars alikofunga mabao 13 msimu uliopita.
Alikumbwa na rungu la kufungiwa mechi 5 na Bodi ya Ligi kabla ya kusimamishwa na klabu yake kwa utovu wa nidhamu.