Mchezaji wa Ghana na klabu ya Berekum Chelsea, Dominic Frimpong ameuawa baada ya basi la timu yake kushambuliwa na majambazi.
Shambulio hilo lilitokea Jumapili wakati timu hiyo ikirejea nyumbani baada ya mchezo dhidi ya Samartex uliochezwa mjini Samreboi, Kusini mwa nchi hiyo.