Skudu Makudubela ametangaza kustaafu soka la ushindani baada ya kudumu kwa miaka 17 kwenye ngazi ya kulipwa

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 hours ago
rickmedia: skudu-makudubela-ametangaza-kustaafu-soka-ushindani-baada-kudumu-kwa-miaka-kwenye-ngazi-185-rickmedia

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga SC, Mahlatse “Skudu – Waziri wa Raha” Makudubela, ametangaza kustaafu soka la ushindani baada ya kudumu kwa miaka 17 kwenye ngazi ya kulipwa. Kupitia Instagram yake, Skudu ameeleza kuwa soka limempa kila kitu ikiwemo nidhamu, urafiki na upendo ambao atauenzi maisha yake yote.

​Katika safari yake, alianza katika Shule ya Ubora ya SAFA Transnet (2004) na kuchezea klabu kubwa za Afrika Kusini kama Mamelodi Sundowns na Orlando Pirates. Kimataifa, alichezea Karviná FK (Czech), FC Gagra (Georgia), Yanga SC (Tanzania), AS Vita Club (DR Congo) na Wiliete FC (Angola).

​Skudu amewashukuru makocha, wachezaji wenzake na mashabiki kwa mchango wao katika mafanikio yake. Anastaafu akijivunia mataji kama MTN8, Telkom Cup na Ligi Kuu ya NBC, huku akitangaza kuhamia rasmi kwenye taaluma ya ukocha.