TRUMP Atangaza Marekani kuanza kuilinda HORMUZ, wengine watalipia

-rickmedia: Rick

Rick

3 days ago
rickmedia: trump-atangaza-marekani-kuanza-kuilinda-hormuz-wengine-watalipia-517-rickmedia

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza rasmi kuwa nchi hiyo itachukua jukumu la kuwa "mlinzi mkuu" wa Mlango-Bahari wa Hormuz, huku akisisitiza kuwa nchi zinazotumia njia hiyo ya kimkakati ya majini zitalazimika kuilipa Marekani kwa gharama za ulinzi huo.

Kupitia ujumbe alayoutuma kwenye mtandao wake wa Truth Social, Rais Trump amebainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuleta usawa wa kiuchumi kulingana na mchango wa kijeshi wa nchi yake katika kulinda usalama wa eneo hilo lenye mivutano mikubwa duniani.

"Kuanzia sasa na kuendelea, Marekani itajulikana kama 'MLINZI WA MLANGO-BAHARI WA HORMUZ'. Hata hivyo, kwa kuzingatia misingi ya USAWA, Marekani itafidiwa tozo ya asilimia 20 (20%) ya shehena zote zinazosafirishwa, ili kufidia gharama zote zinazohitajika katika kuhakikisha ulinzi na usalama kwenye eneo hili hatari zaidi duniani," alisema Rais Trump.