Familia ya marehemu Aslee yadai mwili umerudishwa bila pete

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: familia-marehemu-aslee-yadai-mwili-umerudishwa-bila-pete-601-rickmedia

Baba mzazi wa mrembo aliyefariki Zanzibar Ashlee Jenae, Harry Robinson, anaiambia TMZ kwamba mwili wa Ashlee ulirudishwa kwa familia yao huko New Jersey nchini Marekani siku ya Ijumaa. Baba yake anasema mwili umerudishwa bila vitu vyake pamoja na pete yake ya uchumba, familia haijakabidhiwi kitu chochote cha marehemu Ashlee.

Kwa mujibu wa Harry, familia hiyo haijapewa ratiba ya lini vitu hivyo vitarejeshwa, na anaamini bado viko mikononi mwa wapelelezi kwa sababu kesi hiyo bado ipo Polisi. Pia alieleza kuwa familia imefanya uchunguzi huru wa maiti, ingawa matokeo bado hayajakamilishwa.

Ikumbukwe Ashlee alikuwa Zanzibar kwaajili ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 31 akiwa na mpenzi wake Joe McCann na siku hiyo hiyo alimvisha pete ya uchumba na ndio hiyo ambayo haionekani.

Familia hiyo pia inasema wamekuwa na mawasiliano hafifu na mchumba wa Ashlee, Joe McCann, tangu binti yao afariki. Pia wanafanya kazi ili kupata picha za uchunguzi wa hoteli, wakitumaini kwamba itatoa ufafanuzi zaidi kuhusu saa za mwisho za Ashlee. Wakati huohuo, familia inajiandaa kumpumzisha Ashlee, huku ibada ya mazishi ikitarajiwa kufanyika New Jersey mapema wiki ijayo.