Mrembo Adshlee Jenae afariki kifo cha utata akiwa Vacation Zanzibar

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 hours ago
rickmedia: mrembo-adshlee-jenae-afariki-kifo-cha-utata-akiwa-vacation-zanzibar-81-rickmedia

Familia ya mwanamitandao kutoka Marekani Ashlee Jenae, anayejulikana pia kama Ashly Robinson, inatafuta haki kufuatia kifo cha mrembo huyo cha ghafla alipokuwa mapumziko 'Vacation' kwaajili ya kusheherekea siku yake ya kuzaliwa Zanzibar, Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa Aprili 12, 2026, Ashlee alikuwa amesafiri kwenda Zanzibar kusherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza miaka 31 na alichumbiwa na mchumba wake, Joe McCann, wakati wa safari.

Wawili hao walikuwa wakiishi katika jumba la kifahari huko Zuri Zanzibar kabla ya kifo hakijamkuta aAshlee. Ashlee alikutwa amepoteza fahamu katika jumba walilokuwa wamefikia na kukimbizwa katika hospitali ya eneo hilo ambapo baadaye iligundulika alikuwa amefariki tayari.

Familia yake ilieleza tukio hilo kuwa ni la ghafla na la kuhuzunisha, illieleza kuwa uchunguzi wa kina unaendelea kuhusu mazingira ya kifo chake.