Babalevo ashinda kesi ya Ubunge Kigoma Mjini

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

7 hours ago
rickmedia: babalevo-ashinda-kesi-ubunge-kigoma-mjini-699-rickmedia

Kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma muda mfupi uliopita leo, Alhamisi tarehe 16/07/2026 Mahakama imeifuta kesi ya uchaguzi iliyokuwa imefunguliwa Mahakamani hapo na wananchi wanne (4) waliojitambulisha kuwa wapiga kura wa Jimbo la Kigoma Mjini dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini (CCM) Clayton Revocatus Chipando (Baba Levo)

Uamuzi uliosomwa Mahakamani hapo leo na Jaji Victoria Nongwa aliyekuwa anasikiliza kesi hiyo iliyokuwa inapinga uhalali wa 'Ubunge wa Baba Levo' amesema hoja zote zilizoletwa na walalamikaji ikiwemo hoja za utekaji, madai ya rushwa, udini nk, zimeshindwa kuishawishi Mahakama moja kwa moja kukubaliana kutokana na kwamba ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo umekosa mashiko Mahakama imesema kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na Mahakama kutoka kwa walalamikaji ambao ni wanachama wa ACT Wazalendo, ushahidi uliowasilishwa Mahakamani hapo haina mashiko na kwamba walalamikiwa wote ikiwemo INEC hawana kesi ya kujibu Kwa maamuzi hayo, KESI hiyo imeisha rasmi.