Eng.Hersi Said ateuliwa na BAKITA kuwa Balozi wa kiswahili

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

3 hours ago
rickmedia: enghersi-said-ateuliwa-bakita-kuwa-balozi-kiswahili-857-rickmedia

Bodi ya Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) imemteua Rais wa Yanga SC, Mhandisi Hersi Said kuwa Balozi wa Kiswahili kutokana na uwezo, ushawishi na ushiriki wake kwenye masuala ya kijamii, hususan upande wa michezo.

Mhandisi Hersi atakuwa balozi wa tatu wa BAKITA, ambapo wengine ni Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete na Joram Nkumbi.