Togo imesema itashawishi nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuridhia kutumika kwa ramani ya dunia inayoonesha ukubwa halisi wa Afrika, na kuachana na ya sasa iliyoandaliwa Karne ya 16.
Wakosoaji wanaeleza kuwa ramani ya sasa inayoonesha kuwa Afrika ni ndogo, licha ya ukubwa wa eneo na wingi wa watu, inaathiri masuala ya kielimu, sera na mitazamo juu ya Afrika.