Wizara ya Afya yakanusha video ya Mange Kimambi maiti zikiwa Mochwari

-rickmedia: Rick

Rick

23 hours ago
rickmedia: wizara-afya-yakanusha-video-mange-kimambi-maiti-zikiwa-mochwari-185-rickmedia

Baada kuonekana video inayosambaa kwenye Mitandao ya Kijamii ikionesha Miili ya watu ikiwa imelazwa kwenye Sakafu huku ikidaiwa ni video iliyochukuliwa kwenye Chumba cha kuhifadhia Maiti cha Hospital ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Wizara ya Afya imekanusha Madai hayo na kusema kuwa Video hiyo sio ya Kweli na kwamba imetengenezwa na Wahalifu kwa ajili ya kuzua Taharuki.



Kupitia Barua yao waliochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Wizara ya Afya imeanisha kuwa 'Wizara ya Afya imeona picha ya video inayoonesha miili ya watu ikiwa imewekwa pamoja na kuelezwa kwamba hapo ni Hospitali ya Mwananyamala, Dar es Salaam'.

"Wizara inapenda kukanusha uhalisia wa video hiyo ambayo imetengenezwa na wa-halifu wenye nia ovu ya kuichafua nchi yetu.

Wizara inawataka wote wanaotengeneza picha za kuzua taharuki na kuzihusisha na vituo vya kutolea huduma za afya kuacha mara moja na inawasihi wananchi kuacha kusambaza picha hizo kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja Sheria".

Wizara imehitimisha kuwa "Wananchi mnaombwa kuendelea kuziamini huduma zinazotolewa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zetu kwa kuwa huzingatia weledi unaojali utu na msingi wa maadili ya utabibu"