Bangladesh kupiga kura kesho baada ya mapinduzi ya GenZ kumuondoa Hasina

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: bangladesh-kupiga-kura-kesho-baada-mapinduzi-genz-kumuondoa-hasina-92-rickmedia

Bangladesh inatarajiwa kupiga kura kesho Alhamisi,11, 2026 katika uchaguzi wa kwanza tangu maandamano makubwa yaliyoongozwa na vijana wa kizazi cha Gen Z kumuondoa madarakani aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu, Sheikh Hasina, mwaka 2024.

Kuondoka kwa Hasina huku waandamanaji wakivamia makazi yake kulitikisa siasa za ndani na nje ya nchi hiyo, na kuhamasisha harakati za vijana katika mataifa mengine kama Nepal na Madagascar kupinga rushwa na upendeleo wa kifamilia katika uongozi.

Vijana wengi nchini humo wanaeleza kufurahishwa na kumalizika kwa utawala wa Hasina wa miaka 15, uliokuwa ukikabiliwa na tuhuma za uchaguzi usio huru na wa haki, matumizi mabaya ya rasilimali za umma pamoja na ukandamizaji wa sauti za upinzani.

“Mapinduzi yale yalionyesha nguvu ya Gen Z na kile tunachoweza kufanya,” amesema Mirza Shakil, mwanafunzi aliyeshiriki maandamano ya kumuondoa Hasina madarakani.

Hata hivyo, matumaini ya vijana hao sasa yanakutana na upinzani mkali baada ya wagombea wawili wanaopewa nafasi kubwa ya kuibuka washindi kutotoka katika safu ya walioongoza maandamano hayo.