Ukaribu wa Nicki Minaj na Donald Trump unazidi kuibua sura mpya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

1 day ago
rickmedia: ukaribu-nicki-minaj-donald-trump-unazidi-kuibua-sura-mpya-586-rickmedia

Tukio lisilotarajiwa limekuwa stori kubwa kutokea kwenye Trump Accounts Summit baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kutoa kauli ya utani kuhusu kucha bandia alipokuwa akimtambulisha Nicki Minaj jukwaani.

Trump alisema, “Nilisema nitaacha kucha zangu zikue, kwa sababu nazipenda hizo kucha. Nitaacha kucha zikue!” kauli iliyowachekesha wengi.

Baada ya hapo, Nicki Minaj alipanda jukwaani na kujitangaza wazi kuwa yeye ni shabiki namba moja wa Trump. Tukio hilo lilizidi kushangaza pale ambapo Nicki na Trump walionekana wakishikana mikono mbele ya hadhira.

Ukaribu huu wa Rais Donald Trump na Rapa Nicki Minaj unaibua uasama mkubwa kutoka kwa baadhi ya raia wa Marekani wasiompenda Trump kwenda kwa Nicki Minaj, lakini ni wazi kuwa suala hilo halimsumbui kabisa Nicki Minaj.

Siku kadhaa zilizopita rapa 50 Cent aliweka wazi kuwa yeye hachanganyi mambo ya siasa na dini kwenye kazi zake sababu ameona madhara yake kutoka kwa Nicki Minaj na Kanye West baada ya kuchanganya vitu hivyo.