Wakenya Marufuku kujiunga Jeshi la Urusi kupigana vita Ukraine

-rickmedia: Rick

Rick

2 hours ago
rickmedia: wakenya-marufuku-kujiunga-jeshi-urusi-kupigana-vita-ukraine-459-rickmedia

Serikali ya Kenya imefikia makubaliano rasmi na Urusi kusitisha uandikishaji wa raia wa Kenya kujiunga na jeshi la Urusi katika vita vinavyoendelea nchini Ukraine. Hatua hii inajiri baada ya malalamiko makali kuibuka barani Afrika kufuatia wimbi la vijana wa Kiafrika kushawishiwa kuingia mstari wa mbele vitani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Musalia Mudavadi, alitangaza uamuzi huo baada ya mazungumzo ya faragha na mwenzake wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Moscow. Taarifa zinafichua kuwa zaidi ya Wakenya 1,000 tayari walikuwa wamejiunga, wakivutiwa na mishahara minono ya maelfu ya dola na marupurupu ya zaidi ya $6,000 (takriban KSh 800,000+) kwa wanajeshi wa mkataba.

Pamoja na mvutano huo wa kijeshi, Mudavadi alimiminia sifa uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili, akikumbushia msaada wa Umoja wa Kisovieti wakati Kenya ikijinyakulia uhuru kutoka kwa Waingereza mwaka 1963.