Iran wanasema lengo la vita halijatimia

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: iran-wanasema-lengo-vita-halijatimia-942-rickmedia

Mkuu wa Mahakama ya Iran, Gholamhossein Mohseni Ejei, amesema Tehran imeendelea kusisitiza umuhimu wa kuwa katika hali ya utayari wa asilimia 100 endapo Marekani itaamua kuanzisha mashambulizi mapya, kwa mujibu wa video iliyochapishwa na Vyombo vya Habari vinavyohusishwa na Serikali ya Iran, Fars.

Katika mazungumzo yake, Ejei ameonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa mashambulizi zaidi, akieleza kuwa Marekani bado haijafanikiwa kufikia malengo yake ya kivita licha ya kuwaua baadhi ya Maafisa Wakuu wa Iran katika operesheni zilizopita.

Aidha, katika video nyingine iliyotolewa na Fars, Ejei ameizungumzia hatua ya Marekani kukamata Meli ya mizigo yenye Bendera ya Iran katika Ghuba ya Oman, akieleza kuwa tukio hilo limekiuka makubaliano ya kusitisha mapigano na kuongeza mvutano kati ya pande hizo mbili.

Amesema, “Ni lazima tudumishe utayari wa asilimia 100 kutokana na uwezekano mkubwa wa mashambulizi zaidi, kwani Marekani bado haijafikia malengo yake ya kivita, hatua ya kuweka zuio la Kijeshi Baharini wanayozungumzia ni ukiukwaji wa wazi, na Jamhuri ya Kiislamu bila shaka itajibu.”