Askofu Yvette Flunder, kiongozi mkuu wa kanisa la City of Refuge United Church of Christ na mkuu wa umoja wa makanisa ya The Fellowship of Affirming Ministries, amezua mjadala mzito baada ya kusema kuwa Biblia ina mapungufu makubwa na kuna haja ya kuwa na "Agano la Tatu."
Katika ujumbe wake kwa kituo cha Center for Public Theology & Public Policy, Askofu Flunder ametoa hoja zifuatazo zilizotikisa tasnia ya kidini:
Maandiko "Yenye Shida": Ameeleza kuwa baadhi ya sehemu za Agano la Kale na Jipya ni "problematic" (zenye matatizo), akitolea mfano mistari inayohimiza watumwa kuwatii mabwana zao na inayowataka wanawake kukaa kimya makanisani.
Kukana Uungu wa Agano Jipya: Flunder amesisitiza kuwa Agano Jipya si neno la Mungu, bali ni "maneno kuhusu Mungu." Amesema, "Hili ni jambo la hatari ninalokaribia kusema... Agano J Jipya SI neno la Mungu."
Wito wa Agano la Tatu: Kutokana na kile alichokiita "hasira" yake juu ya jinsi maandiko yanavyomwezea Mungu mwenye chuki, amependekeza kuandikwa kwa Agano la Tatu ili kurekebisha kile anachoamini ni makosa ya kibinadamu yaliyomo kwenye Biblia ya sasa.
Msimamo wa Kidini: Licha ya kauli hiyo, Flunder amesisitiza kuwa yeye ni muumini wa kweli anayemtumaini Mungu kwa moyo wake wote, lakini amewataka watu kuwa tayari "kuchana kurasa" ambazo zinakinzana na haki na utu.
"Watu watasema, 'lakini imo kwenye kitabu.' Nami nitasema, basi tunapaswa kuichana hiyo kurasa." — Askofu Yvette Flunder