Kikwete akutana na Museveni Uganda kujadili hali ya Sudan

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: kikwete-akutana-museveni-uganda-kujadili-hali-sudan-219-rickmedia

Rais Mstaafu wa awamu ya sita ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete ambaye ni Mwakilishi Mkuu wa AU katika Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu amekutana na Rais wa Uganda Yower Museven huko Kampala kujadili hali ya Sudan Kusini.

Kupitia Insta ya Museven aliweka Picha na kuandika kuwa...

"Jioni hii katika Nakasero State Lodge, nilimkaribisha H.E. Jakaya Kikwete, Mwakilishi Mkuu wa AU katika Pembe ya Afrika na Bahari ya Shamu. Tulijadili hali ya Sudan Kusini na kusisitiza umuhimu wa mazungumzo kati ya pande zote."

Uganda itaendelea kuunga mkono juhudi za amani kwani utulivu nchini Sudan Kusini, hasa katika eneo la Ikweta ambako Waganda wengi wanaishi, ni muhimu kwa usalama na ustawi wa kikanda.