Mwanasiasa mkongwe William Vangimembe Lukuvi amefariki Dunia, asubuhi ya Machi 25, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.
Taarifa ya msiba wa Lukuvi aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani imetangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses M. Kusiluka.
Lukuvi ambaye alizaliwa Agosti 15, 1955, alikuwa Bungeni kwa kipindi cha Saba ikiwa ni tangu Mwaka 1995 ulipofanyika Uchaguzi wa Mfumo wa Vyama Vingi nchini.