TRUMP atamba Iran inakaribia kuanza kushindwa Vita

-rickmedia: Rick

Rick

2 hours ago
rickmedia: trump-atamba-iran-inakaribia-kuanza-kushindwa-vita-865-rickmedia

Rais wa Marekani, Donald Trump, amewaambia viongozi wa mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda duniani (G7) kuwa nchi ya Iran "iko ukingoni mwa kusalimu amri," kufuatia mfululizo wa shinikizo kali la kijeshi na kiuchumi kutoka kwa utawala wake.

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na mtandao wa Axios Ijumaa hii, ikinukuu maafisa watatu wa mataifa ya G7 waliofahamishwa kuhusu yaliyojiri katika kikao hicho cha siri kwa njia ya video (virtual meeting) siku ya Jumatano, Trump alionekana mwenye kujiamini kuhusu mustakabali wa mzozo huo.

Kauli hizi za Trump zinakuja wakati kanda ya Mashariki ya Kati ikiwa katika hali ya taharuki kubwa kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani, ambayo yameripotiwa kudhoofisha kwa kiasi kikubwa uwezo wa kijeshi wa Iran na washirika wake nchini Iraq na Syria