Kampuni ya Samsung Electronics Alhamisi hii imezindua mfululizo wake mpya wa simu za Galaxy S26, ikijibu mapigo dhidi ya mpinzani wake mkuu Apple, huku ikipandisha bei za baadhi ya modeli kutokana na gharama kubwa za uzalishaji wa vifaa vya kielektroniki (chips).
Simu hizi mpya zimesheheni mifumo ya kisasa ya Akili Bandia (Gemini ya Google na Perplexity) pamoja na msaidizi wa sauti, Bixby, aliyeboreshwa ili kukabiliana na ushindani wa soko la kidijitali.

chini Marekani, bei ya Galaxy S26 ya kuanzia imepanda kwa 4.7% ($899), huku S26 Plus ikipanda kwa 10% ($1,099). Nchini Korea Kusini, bei imepanda kwa 8.6%, ingawa bei ya modeli ya Ultra haijabadilika.
Modeli ya S26 Ultra inakuja na kioo cha kwanza duniani chenye uwezo wa kuzuia watu wa pembeni kuona unachokifanya (Privacy Display).
Ongezeko la bei linachochewa na uhaba mkubwa wa chips za kumbukumbu (DRAM) duniani. Mahitaji makubwa ya miundombinu ya AI kutoka kwa makampuni kama Meta na Microsoft yamefanya bei za vifaa hivyo kupanda kwa kasi, huku wataalamu wa TrendForce wakitabiri ongezeko la hadi 95% katika robo ya kwanza ya mwaka huu.
Simu hizi zinatarajiwa kuanza kuingia sokoni rasmi kuanzia Machi 11.