Wakazi ahukumiwa kumlipa Baba Levo Milioni 100

-rickmedia: Rick

Rick

4 hours ago
rickmedia: wakazi-ahukumiwa-kumlipa-baba-levo-milioni-100-259-rickmedia

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam imemuamuru Rap Wakazi imlipe Mbunge wa Kigoma Mjini na msanii wa muziki Baba Levo kiasi cha Shilingi Milioni 100 hii ni mara baada ya kumsingizia kuiba simu alizopewa na watu nchini Marekani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Baba Levo ameonesha barua ya hukumu hiyo, huku akikumbushia kesi ilivyoanza. Licha ya hukumu hiyo kutoka Baba Levo anasema kuwa kwa upande wake hafurahishwi kushtakiana mahakamani ila hili ni somo la kutoshadadia mambo ya uongo lenye lengo la kumchafua mtu.