JOHN TERRY Adai kufanyiwa Figisu kwa kukatwa kuwa Benchi la Ufundi Chelsea

-rickmedia: Rick

Rick

3 days ago
rickmedia: john-terry-adai-kufanyiwa-figisu-kwa-kukatwa-kuwa-benchi-ufundi-chelsea-286-rickmedia

Gwiji na nahodha wa zamani wa Chelsea, John Terry, ameweka wazi hisia zake za kukatishwa tamaa baada ya kuachwa nje ya mpango wa usaidizi wa benchi la ufundi wakati wa kipindi cha mpito cha kocha wa muda, Calum McFarlane, mwezi uliopita.

Terry, ambaye kwa sasa anahudumu kama mshauri wa muda katika akademia ya klabu hiyo, ameeleza kuwa alitarajia kuwa sehemu ya msafara uliokwenda kupambana na Manchester City, lakini jina lake lilikatwa katika mazingira anayoyaona kama ya makusudi.

Akizungumza kama mgeni kwenye kipindi cha Golf Life kupitia chaneli ya YouTube ya Jimmy Bullard, Terry alihoji iwapo wamiliki wa klabu au wakurugenzi wa michezo waliamua kumuengua kwa makusudi.

Ikumbukwe kuwa McFarlane alipewa jukumu la kuiongoza timu ya wakubwa baada ya kuondoka kwa Enzo Maresca, hatua iliyomfanya kukabiliana na Pep Guardiola katika dimba la Etihad. Licha ya Terry kufanya kazi kwa ukaribu na McFarlane katika timu za vijana (U21 na U18), hakupandishwa kwenda kusaidia kikosi cha kwanza.

"Sikuwa na hasira, lakini nilikwazika. Nilikuwa sehemu ya kundi la vijana wa U21 waliopandishwa juu, hivyo nilihisi nilitakiwa kuwa sehemu yao hata kama nisingeongoza timu," alisema Terry.

Hadi sasa, uongozi wa Chelsea haujatoa tamko lolote kuhusiana na malalamiko hayo ya Terry.