Uingereza yashtukia michezo michafu ya PUTIN kwenye Vita Iran

-rickmedia: Rick

Rick

2 hours ago
rickmedia: uingereza-yashtukia-michezo-michafu-putin-kwenye-vita-iran-955-rickmedia

Waziri wa Ulinzi wa Uingereza, John Healey, ametoa onyo kali akidai kuwa "mkono wa siri" wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin, unahusika moja kwa moja na mabadiliko ya mbinu za kijeshi zinazotumiwa na Iran na washirika wake.

Kauli hiyo imekuja kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani (drones) lililolenga kambi inayotumiwa na majeshi ya Magharibi huko Erbil, Kaskazini mwa Iraq, usiku wa kuamkia leo.

Akizungumza baada ya kupokea ripoti kutoka kwa maafisa wa kijeshi katika Makao Makuu ya Jeshi la Uingereza (North-West London), Healey alibainisha kuwa marubani wa drones kutoka Iran na vikundi vyenye mfungamano nayo, sasa wanatumia mbinu ambazo zimekuwa zikitumiwa na Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.