VINI Jr awafanya kitu mbaya Benfica, Awapa ushindi Real Madrid nyumbani

-rickmedia: Rick

Rick

2 days ago
rickmedia: vini-awafanya-kitu-mbaya-benfica-awapa-ushindi-real-madrid-nyumbani-587-rickmedia

Katika usiku uliotawaliwa na hisia kali na ujumbe mzito dhidi ya ubaguzi, nyota wa Brazil, Vinícius Júnior, amekuwa shujaa aliyeipeleka Real Madrid hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) baada ya kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Benfica.

Ushindi huo wa Jumanne usiku unamaanisha Real Madrid wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 3-1, huku Vinícius akithibitisha kwanini yeye ni nembo ya klabu hiyo kwa sasa.

Benfica walianza kwa kasi na kusawazisha jumla ya mabao (aggregate) kupitia kwa Rafa Silva dakika ya 14, jambo ambalo lilitikisa uwanja wa Santiago Bernabéu kwa muda.

Kiungo Aurélien Tchouaméni aliirejesha Madrid mchezoni kwa shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Benfica. Zikiwa zimesalia dakika 10 mpira kumalizika, Vinícius alichopoka na walinzi na kupachika bao la ushindi lililozima ndoto za Benfica.

Mchezo huu ulikuwa na uzito wa kipekee kwa Vinícius, siku nane tu baada ya kudai kufanyiwa vitendo vya ubaguzi wa rangi na mchezaji wa Benfica, Gianluca Prestianni, nchini Ureno.

Kabla ya kuanza kwa mchezo, mashabiki wa Real Madrid walinyanyua mabango ya kumuunga mkono nyota huyo, huku ujumbe wa "No to Racism" na "Respect" ukisomwa kwa sauti uwanjani. Vinícius alisherehekea bao lake kwa kucheza densi maarufu pembeni ya kibendera cha kona.