Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa Auwawa Vitani Iraq

-rickmedia: Rick

Rick

3 hours ago
rickmedia: mwanajeshi-mmoja-ufaransa-auwawa-vitani-iraq-748-rickmedia

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amethibitisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa nchi hiyo kufuatia shambulio lililotokea katika eneo la Erbil, Kaskazini mwa Iraq.

Katika taarifa aliyoitoa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter), Rais Macron amemtaja mwanajeshi huyo kuwa ni Afisa Mwandamizi (Chief Warrant Officer) Arnaud Frion, aliyekuwa akitumikia Kikosi cha 7 cha wapiganaji wa milimani (7th Battalion of Chasseurs Alpins) chenye makao yake makuu huko Varces, Ufaransa.