Ilianza minong'ono kuwa mrembo kutoka Kenya, Vera Sidika ana mahusiano ya kimapenzi na msanii Tipsy Gee na sasa sio minong'ono wala siri tena wawili hao wanaonyesha wazi wazi kuwa wapo kwenye mahusiano,suala hili limepokelewa tofauti kidogo na aliyekuwa mpenzi wa Vera Sidika 'Otile Brown' na hajapendezwa nalo.
Kwenye mitandao ya kijamii akaunti mbalimbali zinazopost habari za burudani Kenya zikipost habari hii Otile amekuwa akiacha comments ambazo zinaonyesha wazi kuwa hajafurahishwa na mahusiano haya huku akitamba kuwa kwakuwa wanafuata nyayo zake basi yeye ndio baba yao.

Vera Sidika kuna uwezekano mkubwa anachukizwa na hizi comments za Ex wake na ndio maana yeye pia kupitia ukurasa wake wa Instagrama (InstaStory) ameandika neno moja tu "Move On" jambo lililotafsiriwa kuwa amemlenga Otile Brown sababu anaonekana kumfuatilia sana kwenye penzi lake jipya.

Swali ni je ni kweli bwana Otile Brown ameshindwa kumove-on kwa mrembo Vera Sidika au anaandika hivi makusudi ili na yeye pia aweze kuzungumziwa kama hivi ila hana hisia zozote za kimapenzi na mrembo huyo?
Toa maoni yako kwenye hili.