Mzazi Willy Tuva amjibu shabiki aliyemtuhumu kuua muziki wa Kenya

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 hours ago
rickmedia: mzazi-willy-tuva-amjibu-shabiki-aliyemtuhumu-kuua-muziki-kenya-987-rickmedia

Mmoja kati ya watangazaji walioshiriki kusogeza mbele tasnia ya burudani nchini kenya ni Mtangazaji Mzazi Willy Tuva na hilo ni jambo halipingiki kabisa, sasa kwa baadhi ya watu wa mtandaoni (Keyboard Worriors) huwa hawaoni mchango wa mtu yeyote kwenye kitu chochote wao hua wana kawaida ya kucomment vitu vibaya tu.

Sasa kuna huyu mmoja anayejiita 'Lone Buffalo' huko Instagram ambaye yeye alitokea kusikojulikana na kuacha comment kwenye post ya Mzazi Willy Tuva "Umeua Muziki Wa Kenya' na Willy alimjibu kwa kumuuliza "Hukunialika Mazishini? kwani umekufa? utakuwa nje ya akili yako kwa kusema hivi, fanya uchunguzi na acha kubweka"

Huyu mtu anayetumia jina Lone huko Instagram amefanya watu wengi washangae hii comment yake kwani anamtuhumu mtu ambaye pengine hana uhusika wowote kwenye hicho anachokisema huku wengine wakimuuliza kwani ni Willy aliyeua muziki au wao ndio wamekuwa na kawaida ya kusikiliza muziki mbovu na kuupa nafasi kuliko muziki mzuri.