Yadaiwa ada kubwa ya mkopo yaifanya Kaizer Chief kukataa kumsajili Aziz Ki.

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

4 hours ago
rickmedia: yadaiwa-ada-kubwa-mkopo-yaifanya-kaizer-chief-kukataa-kumsajili-aziz-ki-749-rickmedia

Kwa mujibu wa mchambuzi wa soka barani Afrika, Micky Jnr, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki alipendekezwa kujiunga na klabu ya Kaizer Chiefs katika dirisha la sasa la usajili.

Ripoti zinaeleza kuwa klabu ya Wydad Casablanca ilikuwa tayari kumtoa mchezaji huyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu, kwa masharti ya kulipwa ada ya chini ya dola za Kimarekani 100,000.

Hata hivyo, Kaizer Chiefs walionekana kutoridhishwa na gharama hiyo, wakidai kuwa ni kubwa, jambo lililowafanya kuamua kusitisha mazungumzo ya usajili na kutoendelea na dili hilo.