Jeshi la Marekani limeiteka nyara meli ya mafuta Sagitta inayohusishwa na Venezuela katika Bahari ya Karibi, likidai ilikiuka vikwazo na marufuku ya usafirishaji wa mafuta iliyowekwa na Rais Donald Trump.
Kamandi ya Kusini ya Marekani (SOUTHCOM) imesema hatua hiyo ni sehemu ya operesheni za kuhakikisha mafuta ya Venezuela yanasafirishwa kwa njia halali pekee. Marekani inaendelea kuishutumu Venezuela kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa.