Mfanyakazi wa mgahawa afariki baada ya kudumbukiz a kichwa kwenye mafuta ya moto

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

15 hours ago
rickmedia: mfanyakazi-mgahawa-afariki-baada-kudumbukiz-kichwa-kwenye-mafuta-moto-240-rickmedia



Mfanyakazi mmoja wa mgahawa wa Olive Garden amefariki dunia baada kudumbukiza kichwa chake kwenye kikaango chenye mafuta ya moto tukio hilo lililotokea kazini, katika tawi la Williamsport, jimbo la Pennsylvania, Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star, mfanyakazi huyo (ambaye jina lake halijatolewa) alipata majeraha makubwa na baadaye kukimbizwa hospitali, ambako alifariki kutokana na majeraha hayo.

Idara ya Polisi ya Williamsport imethibitisha tukio hilo na kusema kuwa lilihusishwa na kujiua, lakini imeeleza kuwa haitatoa maelezo zaidi kwa heshima ya marehemu na familia yake.

Afisa Lauren Lesher alisema kuwa mamlaka zinaheshimu faragha ya wahusika na ndiyo sababu ya kutotoa taarifa za kina.Huduma za zimamoto na dharura za Lycoming County zinaonyesha kuwa watoa huduma wa dharura waliitwa eneo la tukio haraka.

Pia, magari mawili ya wagonjwa yalifika kutoa msaada kwa mfanyakazi mwanamke na mteja mmoja waliokuwa wamejeruhiwa kidogo walipokuwa wakijaribu kumsaidia Marehemu.