Nyota wa NFL Stefon Diggs alitoka kwenye Super Bowl LX kwa kupoteza kwenye ubao wa matokeo na maswali yakizunguka kuhusu maisha yake ya kimahusiano na Cardi B.
Sasa 50 Cent hakupoteza muda kabisa. Muda mfupi baada ya New England Patriots kushindwa kwa matokeo ya 29-13 na Seattle Seahawks, 50 Cent alishiriki chapisho kwenye Instagram ambalo liliweka usiku wa Diggs kama pigo mara mbili.
50 Cent aliandika. "Je, unaweza kufikiria kuamka asubuhi hii na umepoteza gemu ya Super Bowl, na umempoteza mpenzi wako". Ingekuwa mimi ningemwambia kila mtu akae mbali na mimi, niywe na niende zangu kulala tu. LOL."
Diggs alivumilia usiku wa kutatanisha wa Super Bowl huku timu yake ikijitahidi kuendana na kasi ya Seattle. Lakini matokeo yalikuwa ni kipigo kikali. Mbaya zaidi mambo yalibadilika haraka kutokana na uvumi wa uhusiano wake na Cardi B kufika tamati.
50 Cent akikuamulia hakika atakuganda mpaka uhisi hujificha sayari nyingine.