Cardi B na Steflon Giggs penzi lao limeota mbawa kwenye fainali za Super Bowl

-rickmedia: Saraphina Jerry

Saraphina Jerry

2 days ago
rickmedia: cardi-steflon-giggs-penzi-lao-limeota-mbawa-kwenye-fainali-super-bowl-106-rickmedia

Cardi B na Stefon Diggs wametengana, unaambiwa jambo hili lilitokea kwenye fainali za Super Bowl ambapo Cardi B alimwona mama mtoto wa Stefflon kwenye siti za mbele kwenye mchezo huo huku yeye akiwa sehemu nyingine. Cardi B aliondoka kabla ya mchezo kumalizika na aliisusia mpaka hagfla (After Party) aliyokuwa amemuandalia Stefflon aliyotumia gharama nyingi kuiandaa na hakuna hata mmoja kati yao aliyehudhulia.

Mpaka sasa hakuna anayemfata mwenzake Instagram (Kum-Follow).

Cardi B amethibitisha kuwa single kwenye live aliyoingia baada ya kuondoka mapema kwenye fainali la Super Bowl.

Cardi B pia ametupa dogo kwa Stefflon Diggs kupoteza kwenye fainali ya America Football katika SuperBowl, kasema ana watoto wengi kuliko kushika mpira kwenye mchezo wa fainali za Super Bawl.

Cardi B na Stefon walipata mtoto wao wa kwanza pamoja November 2025, ni mtoto wa nne kwa Cardi B, na wa 5 kwa Diggs mwenye watoto 6, Cardi alipata ujauzito kabla ya talaka yake na Offset kukamilika kitu kilichozua gumzo mitandaoni.